JE WAJUA

DJ R GUY

DJ FERUUH

Kasumal Rashid aanza kuingia katika fani ya Udj katika mji wa Kigoma, apewa mafunzo na DJ R GUY dj mkongwe wa Radio moja iliyopo jijijni Dar es saalam ijulikanayo kama KISS FM. Kasumal aanza mafunzo hayo katika Lounge & Club maarufu iliyopo mjini Kigoma ijulikanayo kama THE WALLET, ametokea kuipenda kazi hiyo kwa kupitia DJ maarufu nchini Tanzania anaefanya kazi katika Redio moja maarufu nchiniTanzania iitwaayo CLOUDS MEDIA GROUP (CMG). Dj huyo anajulikana kama DJ FERUUH, na Dj Feruuh amekuwa akimsapoti sana Kasumal katika kila hatua na kikwazo akikutacho mbele yake kwani amekuwa akimpa moyo pia nakumtaka afanye bidii kwani  ameweza kumsaidia kumtafutia Dj mzuri anaepatikana katika mji wa Kigoma na mwenye uwezo mzuri. Na sasa Kasumal ameanza kuwa katika moja ya madj nchini Tanzania na dunia kwa ujumla, na kwa sasa katika fani hiyo anajiita kama DJ VAN  

Post a Comment

0 Comments