FAHAMU VIONGOZI NA MAJUKUMU YAO

Watanzania wengi wamekuwa wengi wa kuongea bila ufahamu wa mambo waongeayo, leo nipende kuwajuza kuhusu utambuzi wa viongozi wao na majukumu yao. Kutokana na swala hili tutaweza kufahamu kiongozi bora na bora kiongozi katika maeneo yetu na taifa kwa ujumla, nipende kuanza na:-

1. Serikali ya mtaa/ kijiji
Serikali ya mtaa/ kijiji ni nini ?
Ø Ni chombo cha utawala wa umma, kilichopewa madaraka ya kuamua na kuendesha shughuli za kimaendeleo katika mtaa/kijiji
Majukimu ya serikali ya kijiji/ mtaa
(i) Kulinda na kutunza utulivu na amani na kusimamia utawala bora
(ii) Kuendeleza ustawi wa jamii na kuinua uchumi wa wananchi wake ikiwemo kuimalisha afya, elimu, utamaduni, burudani na ustawi wa wananchi
(iii) Kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana kwa mujibu wa sera za maendeleo mijini na vijijini
(iv) Kuhakikisha na kuchukua hatua zozote zinazofaa katika kuzuia au kuondoa uhalifu na kulinda watu pamoja na mali zao
(v) Kuimalisha kilimo, viwanda, na biashara
(vi) Kuondoa umasikini na kero nyingine katika jamii hususani kwa kuzingatia makundi ya vijana, wazee na wasiojiweeza
(vii) Kuhimiza dhana ya ushirikishwaji wa wananchi, vyama vya hiari na visivyo vya hiari katika kujiletea maendeleo
(viii) Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato vya kuwezesha halmashauri kutekeleza majukumu yake

Mwananchi
Ø Ni raia mwenye uraia halali wa eneo husika
Majukumu ya Mwananchi
(i) Kuhudhuria mikutano yote katika kitongoji, kijiji/mtaa na kuhakikisha kuwa mikutano inafanyika kila baada ya muuda uliopangwa
(ii) Kulinda mali, rasimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu ikiwemo ubadhirifu, wizi, rushwa,na mengineyo
(iii) Kumwondoa kiongozi au viongozi wasiowajibika kwa kumpigia kura ya hapana
(iv) Kujenga na kuimarisha mshikamano uliopo katika jamii yake
(v) Kushriki, kupanga, kusimamia na kuthamini na kuhoji matokeo ya miradi yote katika kitongoji, kijiji/mtaa
(vi) Kushriki katika kupiga na kupigiwa kura, kugombea nafasi za uongozi
(vii) Kuheshimu kiongozi au viongozi wake
(viii) Kujua kuhusu mapato na matumizi ya fedha za kitongoji, kijiji/mtaa
(ix) Kushiriki katika shughuri zote za kisiasa katika kijiji/mtaa na kitongoji chake
(x) Kushirikishwa na kiongozi wake katika shughuri mbalimbali za maendeleo
(xi) Kujua mipango mbalimbali ya maendeleo inayoendeshwa  katika kitongoji na kijiji chake au mtaa
(xii) Kuhakikisha kiongozi wake aliemchagua anatimiza wajibu wake ipasavyo
(xiii) Kudai haki zake za msingi kutoka kwa kiongozi wake
(xiv) Kuelewa sheria zote zilizopo katika kitongoji na kijiji au mtaa wake na kuishi kwa kufuatana na sheria hizo
(xv) Kutambua nafasi yake katika jamii ili aweze kushiriki katika shughuri mbalimbali za maendeleo
(xvi) Kutoa taarifa za vitendo viovu kama rushwa, ubadhilifu na wizi katika ngazi husika kama polisi, afisa mtendaji wa kijiji/mtaa.
  
Viongozi wa serikali ya mtaa/ kijiji na majukumu yao
Wafuatao ni viongozi wa serikali ya mtaa/ kijiji
Mjumbe wa halmashauli ya serikali ya mtaa/ kijiji
Ø Ni mwakiilishi wa wananchi katika kikao cha halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji
Majukumu ya Mjumbe wa halmashauli ya serikali ya mtaa/ kijiji
(i)  Huchaguliwa na wakazi wa kijiji/mtaa katika uchaguzi mkuu wa wa serikali za mtaa/kijiji
(ii) Kushauri na kutoa maoni katika vikao vya halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji
(iii) Kuhudhuria vikao vyote vya halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji
(iv) Ni muhusika na mpangaji, utekelezaji na utendaji wa shughuri za kijiji/mtaa
(v) Ni kiungo cha halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji na wanakijiji/wakazi wa mtaa
(vi) Wanawajibika kwa mkutano mkuu wa kijiji/mtaa

Mwenyekiti wa kitongoji
Ø Ni kiongozi wa kitongoji
Majukumu ya Mwenyekiti wa kitongoji
(i) Huchaguliwa na wakazi wa kitongoji katika uchaguzi mkuu wa wa serikali za mtaa/kijiji
(ii) Ni mjumbe wa halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji kwa wadhifa wake
(iii) Ni kiongozi mwa viongozi wa mtaa/kijiji
(i) Ni kiungo kati ya halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji na wakazi wa kitongoji
(iv) Kuimarisha umoja na ushikamano kati ya serikali ya mtaa/kijiji na wanamtaa/wanakijiji
(v) Kuwasilisha maoni,mapendekezo na mahitaji ya kitongoji kwa halmashauri ya mtaa/ kijiji
(vi) Kuitisha mikutano ya wakazi wa kitongoji pale anapoona inafaa
(vii) Mikutano ya kitongoji haina uwezo wa maamuzi inaendeleza mijadala na kuandaa maoni na mapendekezo tu
(viii) Kuwasilisha taarifa za halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji kwa wakazi wa kitongoji
(ix) Kutunza rejista ya wakazi ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusumaendeleo ya kitongoji kwa ujumla ikiwa ni pamoja kumbukumbu za vizazi na vifo
(x) Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la kitongoji
(xi) Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa halmashauri ya kijiji/mtaa
(xii) Kusimamia katika eneo lake suala zima la hifadhi ya mazingira hususani vyanzo vya maji
(xiii) Kusimamia suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja utekelezaji wa kampeni za afya za kitaifa, kimkoa au kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na hasa vita dhidi ya UKIMWI
(xiv) Kusimamia utekelezaji wa kanuni za kilimo na ufugaji bora ili kuinua hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji
(xv) Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na kushirikiana na viongozi wa shule katika kudhibiti utoro shuleni
(xvi) Kuhamasisha elimu ya watu wazima
(xvii) Kusimamia na kuhamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea
(i) Kusuruhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha kamati ya kijiji au kupelekwa kwenye balaza la kata au mahakama
(ii) Kuwakilisha kitongoji katika serikali ya kijiji
(iii) Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za taifa na mikutano ya hadhara.
(iv) Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na halmashauli ya kijiji, wilaya, mji, manispaa au jiji

Mwenyekiti wa mtaa/ kijiji
Ø Ni kiongozi wa halmashauli ya serikali ya mtaa/kijiji
Majukumu ya Mwenyekiti wa mtaa/ kijiji
(i) Ni mwenyekiti wa mkutano mkuu wa halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji akisaidiwa na mtendaji wa kijiji
(ii) Kupanga ratiba za vikao, kuandaa na kuitisha vikao vya mkutano mkuu wa halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji
(iii) Kusimamia na kuwajibisha kamati tendaji
(iv) Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya fedha za kodi, ushuru na mapato mengine ya mtaa/kijiji
(v) Ni mkuu wa serikali ya kijiji/mtaa
(vi) Ni mwakilishi wa kijiji kwenye kamati ya maendeleo ya kata
(vii) Kutoa huduma kwa usawa kwa wanakijiji wote bila kujali tofauti za kisiasa, kijinsia au za kidini
(viii) Atakuwa mfano wa uongozi na utendaji bora wa kazi zake katika jamii.
(ix) Kusuruhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha kamati ya kijiji au kupelekwa kwenye balaza la kata au mahakama
(x) Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa halmashauri ya kijiji/mtaa

2. Serikali kuu
Serikali ya kuu ni nini ?
Ø Ni chombo cha utawala wa umma, kilichopewa madaraka ya kuamua na kuendesha shughuli za kimaendeleo katika kata, jimbo na taifa kwa ujumla

Viongozi wa serikali kuu
Wafuatao ni viongozi wa serikali kuu na majukumu yao
Mtendaji wa mtaa (MEO)/ kijiji (VEO)
Ø Ni mwakilishi na mwajiriwa wa halmashauli ya wilaya katika halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji.
Majukumu ya Mtendaji wa mtaa (MEO)/ kijiji (VEO)
(i) Ni mtendaji wa shughuli zote za mtaa/ kijiji
(ii) Mtunzaji wa kumbukumbu zote za mtaa/ kijiji za vikao vya mtaa/kijiji pamoja na hati ya kuandikishwa mtaa/kijiji, mali za mtaa/kijiji, rejesta ya mtaa/kijiji na barua zote
(iii) Ni mwajiriwa wa halmashauri ya wilaya, huwajibika kwa halmashauri ya wilaya na huwajibika pia kwa halmashauri ya serikali ya mtaa/kijiji
(iv) Ni mshauri mkuu wa wananchi na muhamasishaji wa utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo ya mtaa/kijiji
(v) Ni mwasilishaji wa taarifa zote muhimu za mtaa/kijiji kwa afisa mtendaji wa kata (WEO)
(vi) Ni mlinzi wa amani ( Anaweza kumkama mtu yeyote anaeonekana kuhatarisha amani katika mtaa/kijiji chake)
(vii) Msimazi wa utekelezaji wa sheria ndogo katika mtaa/kijiji chake
(viii) Kupanga na kuhakikisha kupitishwa ratiba za vikao vya mkutano mkuu na halmashauri ya mtaa/kijiji
(ix) Kuandaa ajenda za vikao mbalimbali kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa/kijiji
(x) Kuandaa taarifa mbalimbali za halmashauri ya mtaa/kijiji au kamati ya mtaa/kijiji, au mkutano mkuu wa kijiji/mtaa, pamoja  na makisio na hesabu za mapato na matumizi
(xi) Kuwashauri wenyeviti wahusika juu ya taratibu za kuendesha vikao, kufanya maamuzi na kuandika mihutasari ya vikao na kuhifadhi katika daftari
(xii) Kufanya mawasiliano na ngazi zingine za utawala kwaniaba ya kijiji/mtaa
(xiii) Ni msimamizi wa mapato na kodi za kijiji/mtaa
(xiv) Msambazaji wa habari na taarifa mbalimbali kijijini/mtaani
(xv) Kuwa daraja kati ya kijiji/mtaa na asasi zingine kijijini/mtaani au nje ya mtaa/kijiji chake kama zahanati, shule, mashirika yasio yakiserikali
(xvi) Mfuatiliaji wa miradi ya kijiji/mtaa na kutoa taarifa kwenye halmashauri ya kijiji au kamati ya mtaa
(xvii) Mfuatiliaji wa utekelezaji wa maamuzi ya vikao mbalimbali vya kijiji/mtaa
(xviii) Muandaaji wa semina warsha za wanakijiji/wakazi wa mtaa na viongozi wa mtaa/kijiji
(xix) Hufanya lolote linalofaa kuboresha utawala na utendaji wa serikali ya kijiji/mtaa

Mtendaji wa kata (WEO)
Ø Ni mwakilishi na mwajiriwa wa halmashauli ya wilaya katika kata
Majukumu ya Mtendaji wa kata (WEO)
(i) Ni mtendaji mkuu wa kata na kiungo cha uongozi kwa idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
(ii) Atakuwa muhamasishaji mkuu wa umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji mali, kuondoa njaa na umasikini
(iii) Atakuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya kata
(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuri za maendeleo ya kata, vijiji na mitaa
(v) Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika kata yake, atamsaidia mkurugenzi kuratibu na kusimamia shughuli za uchaguzi katika kata
(vi) Kumsaidia na kumwakilisha mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake
(vii) Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya kata
(viii) Kuandaa na kuratibu taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa katibu tarafa
(ix) Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vijiji/mtaa na NGOs
(x) Atakuwa msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa  katika vijiji/mitaa, vitongoji na kata yake

Diwani viti maalumu
Ø Ni kiongozi msaidizi wa diwani aliechaguliwa na chama cha siasa
Majukumu ya Diwani viti maalumu
(i) Kuwakilisha wanachi katika halmashauri ya wilaya au manispaa ya mji
(ii) Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa halmashauri
(iii) Kusimamia matumizi ya fedha za halmashauri
(iv) Kuwa kiungo kati ya halmashauri na ngazi za misingi za serikali za vijiji/mitaa
(v) Kuhamasisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umasikini, afya na elimu
(vi) Kuzingatia misingi yote ya utawala bora
(vii) Ni mjumbe katika vikao vya halmashauri

Diwani
Ø Ni mwakilishi wa wananchi ngazi ya kata aliyechaguliwa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali za vijiji/mtaa.
 Majukumu ya diwani
(viii) Kuwakilisha wanachi katika halmashauri ya wilaya au manispaa ya mji
(ix) Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa halmashauri
(x) Kusimamia matumizi ya fedha za halmashauri
(xi) Kuwa kiungo kati ya halmashauri na ngazi za misingi za serikali za vijiji/mitaa
(xii) Kuhamasisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umasikini, afya na elimu
(xiii) Kufuatilia utekelezaji wa mipango yote ya wananchi na ya halmashauri
(xiv) Kutetea maamuzi ya halmashauri
(xv) Kuzingatia misingi yote ya utawala bora
(xvi) Ni mjumbe katika vikao vya halmashauri
Wajibu wa Diwani
(i) Kuangalia na kutambua shida zinazowakabili wananchi wake
(ii) Kuwaheshimu wananchi wake
(iii) Kushirikiana na wanachi wake katika kazi mbalimbali za kujenga taifa
(iv) Kushirikiana na viongozi wa sehemu yake, wilaya na mkoa wake
(v) Kuisaidia serikali itawale vizuri
(vi) Kuhudhuria mikutano ya halmashauri

Meya/Mwenyekiti wa halmashauli ya wilaya
Ø Ni kiongozi wa balaza la madiwani aliechaguliwa na madiwani wa kata zote katika manispaa/ wilaya
 Majukumu ya Meya/Mwenyekiti wa halmashauli ya wilaya
(i) Ni kiongozi mkuu wa halmashauri ya wilaya/manispaa mwenye dhamana ya kisiasa
(ii) Ni mwenyekiti wa baraza la madiwani na kamati ya kudumu ya fedha na mipango/utawala
(iii) Ni mtia lakiri/muhuri katika nyaraka zote rasmi za halmashauri
(iv) Kuthibiti na kuongoza mikutano ya baraza la madiwani ili liweze kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wananchi wote wa halmashauli ya wilaya/manispaa
(v) Kuwa ofisini ambapo ni wilayani kwa kukutana na wananchi wa wilaya/manispaa yake wenye shida, kero na maoni ya kuboresha utendaji wa halmashauri mara mbili kwa wiki.

Katibu tarafa
Ø Ni mwakilishi na mwajiriwa wa halmashauli ya wilaya katika tarafa
Majukumu ya Katibu tarafa
(i) Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa
(ii) Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya
(iii) Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa
(iv) Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa
(v)  Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake
(vi) Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo
(vii) Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
(viii) Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya
(ix) Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake
(x) Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(xi) Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
(xii) Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa
(xiii) Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
(xiv) Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri
(xv) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
(xvi)  Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji
(xvii) Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.
(xviii) Kuwa Katibu wa vikao vitakavyowahusisha Watendaji Kata, Madiwani na Wataalam waliopo katika eneo lake;
(xix) Kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Madiwani la Halmashauri na kutoa ushauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanyika katika eneo lake;
(xx) Kushiriki kama mjumbe kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Wilaya DCC;

Mbunge viti maalumu
Ø Ni kiongozi msaidizi wa mbunge aliechaguliwa na chama cha siasa
 Majukumu ya Mbunge viti maalumu
(i) Kuwakilisha wananchi wa jimbo lake bungeni
(ii) Kuunganisha watu wake na serikali
(iii) Kukusanya shida, kero na maoni ya watu wake na kurudisha majibu
(iv) Kutunga sheria mpya
(v) Kuisahihisha serikali ili itie juhudi zake zote kutimiza hoja za watu

Mbunge
Ø Ni mwakilishi wa jimbo katika lake katika chombo kikuu cha jamhuri ya muungano ambacho kinamadaraka, kwaniaba ya wananchi kusimamia na kushauri serikali ya jamhuri ya muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
 Majukumu ya Mbunge
(vi) Kuwakilisha wananchi wa jimbo lake bungeni
(vii) Kuunganisha watu wake na serikali
(viii) Kukusanya shida, kero na maoni ya watu wake na kurudisha majibu
(ix) Kutunga sheria mpya
(x) Kuisahihisha serikali ili itie juhudi zake zote kutimiza hoja za watu
Wajibu wa mbunge
(vii) Kuangalia na kutambua shida zinazowakabili wananchi wake
(viii) Kuwaheshimu wananchi wake
(ix) Kushirikiana na wanachi wake katika kazi mbalimbali za kujenga taifa
(x) Kushirikiana na viongozi wa sehemu yake, wilaya na mkoa wake
(xi) Kuisaidia serikali itawale vizuri
(xii) Kuhudhuria mikutano ya bunge

Mkuu wa wilaya
Ø Ni kiongozi wa wilaya aliyeteuliwa na raisi, kwa kumwakilisha raisi katika wilaya
Majukumu ya Mkuu wa wilaya
(i) Kusimamia kamati ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Wilaya
(ii) Kusimamia na kutekeleza ilani ya chama
(iii) Kupokea wageni mbalimbali
(iv) Kupokea mwenge
Katibu tawala wilaya
Ø Ni mtendaji na afisa maduhuli wa wilaya
Majukumu ya Katibu tawala wilaya
(i) Ni masaidizi na mshauri mkuu wa mkuu wawilaya na ndiye mtendaji mkuu kwenye ofisi ya mkuu wa wilya
(ii) Ni msimamizi mkuu/afisa masuhuli wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya mkuu wa wilaya  na mganga mkuu wa mkoa.






Mkurugenzi
Ø Ni mtendaji mkuu wa serikali katika halmashauri.
Majukumu ya Mkurugenzi
(i) Ni msimamizi wa usalama na amani katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri 
(ii) Kuweka saini nyaraka mbalimbali za Halmashauri
(iii) Kupokea na kusikiliza matatizo ,changamoto na au malalamiko ya wananchi kwenye Halimashauri husika
(iv)  Ni afisa Uhusiano na Msemaji Mkuu wa maamuzi ya Halmashauri
(v) Ni msemaji Mkuu wa maamuzi na maazimio ya Halmashauri
(vi) Kuitisha na kuendesha mikutano ya menejimenti ambapo mambo mbalimbali ya Halmashauri yatajadiliwa na kutolewa uamuzi
(vii) Kutayarisha rasimu za ajenda za mikutano ya Kamati zitakazokutana kila mwezi ,taarifa na mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye mkutano wa Halmashauri au Kamati ya Fedha, n.k.
(viii) Kuratibu Idara zote za Halmashauri na kuratibu utekelezaji wa majukumu na kazi za Halmashauri
(ix) Kuchukua hatua za kinidhamu kwa wakati na kwa mujibu wa sheria
(x) Kubuni sera na mipango ya Maendeleo ya Halmashauri na Kusimamia na kutekeleza sera, mipango na maamuzi ya Halmashauri
(xi) Kushauriana na kujadiliana na Mwenyekiti/Meya wa Halimashauri mara kwa mara juu ya masuala mbalimbali ya Halmashauri hasa yale yanayoweza kuleta athari za kisiasa na mara nyingine kushauriana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali katika eneo la Halmashauri husika ili kuhakikisha kuwa mfumo wa Serikali za Mitaa kwenye ngazi za jamii unafanya kazi na kuchukua hatua haraka.
(xii)  Ni Katibu wa Mikutano ya Halmashauri na ana majukumu ya Kutayarisha ajenda ya mikutano ya Baraza/Kamati akimshirikisha Mwenyekiti/Meya
(xiii) Kutoa au kutuma mihutasari na nyaraka mbalimbali kwa Madiwani na kwa Mkuu wa Mkoa na Wilaya kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halimashauri
(xiv) Kuandika mihutasari ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mikutano mbalimbali ya Halimashauri
(xv) Ni afisa Masuuli (Accounting Officer)

Mkuu wa mkoa
Ø Ni kiongozi wa mkoa aliyeteuliwa na raisi, kwa kumwakilisha raisi katika mkoa
Majukumu ya Mkuu wa mkoa
(i) Kuhakikisha uwepo wa Haki na Sheria katika mkoa
(ii) Kuongoza na kusimamia operesheni za Maafa na Kufariji
(iii) Kufanya jitihada za kuhakikisha kutimizwa kwa sera za serikali juu ya Mkoa husika.
(iv)  Kufanya yale yote yatakayosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano na serikali za mitaa.

Katibu tawala mkoa
Ø Ni mtendaji na afisa maduhuli wa mkoa
Majukumu ya Katibu tawala mkoa
(i) Ni masaidizi na mshauri mkuu wa mkuu wa mkoa na ndiye mtendaji mkuu kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa 
(ii) Ni msimamizi mkuu/afisa masuhuli wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya na mganga mkuu wa mkoa.

Naibu waziri
Ø Ni kiongozi wa serikali alieteuliwa na raisi kumsaidia kusimamia waziri mwenye wizara husika
Majukumu ya Naibu waziri
(i) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(ii) Kusimamia wizara kiutendaji na kimaendeleo
(iii) Kupokea kero, matatizo na maoni kutoka kwa wabunge
(iv) Kutatua kero na matatizo ya wananchi kitaifa
(v) Kuleta maendeleo katika taifa
(vi) Kumsaidia waziri majukumu
(vii) Ni mtendaji wa serikali katika wizara husika
(viii) Kuwajibisha viongozi wa serikali

Waziri
Ø Ni kiongozi wa serikali alieteuliwa na raisi kusimamia wizara husika
Majukumu ya Waziri
(ix) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(x) Kusimamia wizara kiutendaji na kimaendeleo
(xi) Kupokea kero, matatizo na maoni kutoka kwa wabunge
(xii) Ni mjumbe katika kikao cha mawaziri
(xiii) Kutatua kero na matatizo ya wananchi kitaifa
(xiv) Kuleta maendeleo katika taifa
(xv) Ni mtendaji wa serikali katika wizara husika
(xvi) Kuwajibisha viongozi wa serikali

Waziri mkuu
Ø Ni kiongozi wa serikali alietuliwa na raisi kuongoza na kusimamia wizara kwa kupigiwa kura na wabunge.
Majukumu ya Waziri mkuu
(i) Kusimamia wizara kiutendaji na kimaendeleo
(ii) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(xvii) Kupokea kero, matatizo na maoni kutoka kwa wabunge
(iii) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(iv) Kuteuwa na kufukuza viongozi wa serikali
(v)  Ni makamu wa raisi baada ya raisi na makamo wa raisi kutokuepo katika taifa
(vi) Ni mtendaji wa juu wa taifa
(vii) Kuwajibisha viongozi wa serikali

Makamu wa Raisi
Ø Ni kiongozi wa serikali msaidizi wa raisi aliechaguliwa na chama cha siasa.
Majukumu ya Makamu wa Raisi
(i) Ni kiongozi wa serikali
(ii) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(iii) Kuwakilisha taifa katika mikutano ya umoja wa mataifa, umoja wa nchi zilizopo jangwa la sahara na umoja wa nchi za Afrika baadala ya Raisi
(iv) Kuwajibisha viongozi wa serikali
(v) Kuhamasisha maendeleo katika taifa
(vi) Kuhamasisha vita dhidi ya Umasikini, Afya na Ujinga ki taifa

Raisi
Ø Ni kiongozi mkuu wa serikali aliechaguliwa na wananchi kuongoza nchi.
Majukumu ya Raisi
(i) Ni kiongozi wa nchi
(ii) Amri jeshi mkuu
(iii) Kutekeleza ilani ya chama kiutendaji na kimaendeleo katika taifa
(iv) Kuteuwa wakurugenzi wa halmashauri, katibu tawala wa wilaya, katibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri na waziri mkuu.
(v) Kuwakilisha taifa katika mikutano ya umoja wa mataifa, umoja wa nchi zilizopo jangwa la sahara na umoja wa nchi za Afrika
(vi) Kuteuwa na kufukuza viongozi wa serikali
(vii) Kusaini mikataba ya kitaifa
(viii) Kusaini miswada ya sheria kuwa sheria
(ix) Kutoa misamaha kwa wafungwa
(x) Ni mlezi wa wananchi katika taifa
(xi) Ni mwenyekiti wa vikao vya balaza la mawaziri

Makala haya yameandaliwa na raia mwema na mzalendo wa taifa lake na kufanikishwa kwa ushirikiano wa machapisho kutoka : Ofisi ya waziri mkuu-tawala za mikoa na serikali za mitaa
Jina la Mwandishi : KASUMAL RASHID SALEHE
Taaluma :     Teknolojia habari na mawasiliano ( TEHAMA ) 
Mawasiliano :  0673747573