Na:Kasumali Rashidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema mwaka huu wa fedha Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kuimarisha huduma za uzazi salama Zanzibar ikiwa ni moja ya kipaumbele chake kikubwa.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo katika mbio fupi na yeye mwenyewe kushiriki matembezi ya hiari ya kampeni ya Uzazi ni Maisha yaliyoanza Kiembe Samaki na kumalizika viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewashukuru Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari(Mobile van) ambalo litakuwa msaada muhimu kwa Wizara ya Afya kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kusafirisha wataalamu, sampuli na kutoa huduma za upimaji pamoja na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo mbalimbali vya afya Zanzibar.
Vilevile, Rais Dk.Mwinyi
amefurahishwa kusikia kwamba kampeni ya Uzazi ni Salama ilioandaliwa na Shirika la Amref Health Africa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya itakuwa ya miaka mitatu mfululizo na imeanza tangu mwaka 2022 na itamalizika mwaka 2024 kwa lengo la kukusanya shilingi Bilioni moja kwa madhumuni ya kununulia vifaa tiba katika hospitali kusaidia uzazi salama na kuimarisha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito kabla na baada ya kujifungua

0 Comments
Karibu!