​
Na: Kasumal Rashid
Kata ya Kalya ni kata inayopatikana tarafa ya Buhingu, wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Kata hii ina vijiji sita ambavyo ni:-
1. Ubanda
2. Lufubu
3. Kashagulu
4. Tambusha
5. Kalya
6. Sibwesa.
Kata hii inahuduma zote muhimu za kijamii kama vile maji, umeme, usafiri, elimu, afya pamoja na kilimo na ufugaji. Japo kuwa na huduma hizo zote, bado wananchi wanaendelea kuwa na shida ya kupoteza haki zao kwa kukosa eneo la msaada wa kisheria, kwani kutoka kata ya Kalya mpaka wilayani Uvinza ni umbali wa kilomita 300. Hivyo kufanya wananchi kushindwa kufika katika ofisi za wilaya kwa lengo la kupata huduma, vilevile wananchi wa kata ya Kalya ni wahanga wa kupoteza haki zao kwa kukosa mahakama.
Kata ya Kalya imekuwa na jengo la mahakama tangu miaka ya 80, lakini chakushangaza mpaka sasa huduma haitolewi tangu miaka ya 2000, ambapo ni wakati wa muda wa mahakama za kutembea. Kukosa huduma hizo kumefanya wananchi wengi wapoteze haki zao kwa kusingiziwa, na hata kuombwa rushwa baada ya kutishwa.
Jiunge na Kasumal kwa group laWhatsApp kwa kubonyeza kiungo hicho hapo chini
https://chat.whatsapp.com/ByV1LHmUcY96NPspOfXgak
0 Comments
Karibu!