FURSA YAGEUKA KUWA ADHABU KWA WANANCHI

Kilimo cha umwagiliaji kijiji cha KashaguluNa: Kasumal Rashid

Kijiji cha Kashagulu ni miongoni mwa vijiji vinavyopatikana kata ya Kalya, kijiji cha Kashagulu kinajihusisha na kilimo cha biashara na chakula nacho ni  Mpunga. 

    Wananchi wa kijiji cha Kashagulu wanatumia mradi wa umwagiliaji, kwa muda wote na miaka yote tangu mwaka 2018 mradi huo ulipokamilika, japo na kuutumia lakini wamejikuta katika hali ngumu ya kiundeshaji kwa sababu zifuatazo:-

1. Mradi kuendeshwa na wakulima.

    Wakulima wanasema moja ya eneo ngumu, ni namna ya uendeshaji wa mradi huo wa umwagiliaji sababu mradi hauna mtaalamu wala kiongozi wa serikali ngazi ya kijiji, bali unaendeshwa na wakulima wenyewe. Wanakijiji wanapata tabu sana pale wanapoona viongozi wa serikali hawajihusishi na mradi huo na kufanya viongozi wa umoja wa wakulima ndio wanakuwa vinara, wakati hata baadhi ya mipango hujiamulia viongozi wenyewe. Vile vile uchaguzi wa viongozi hao wa umoja wa wakulima huendeshwa bila kufuata taratibu za uchaguzi kwani wananchi wanasema uchaguzi huwa hauzingatii katiba wala kanuni bali matakwa ya mtu.

2. Tozo kwa wananchi. 

    Moja ya eneo linalowapa ugumu na ukakasi wananchi ni eneo la tozo, kwani tozo zinazokusanywa hukusanywa na uongozi wa umoja wa wakulima, ikiwa hakuna hata kiongozi mmoja wa serikali. Wananchi wanasema tozo zenyewe huwa ni shilingi elfu kumi na tano kwa heka moja.

Hayo ni machache kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Kashagulu

Post a Comment

0 Comments