Na: Kasumal Rashid
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mheshimiwa Dk.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuasisi wazo la kuwa na Tamasha la Kizimkazi kwa madhumuni ya kuimarisha umoja, mshikamano na kudumisha mila na utamaduni ili kuchochea uzalendo na kuhamasisha shughuli za maendeleo ya wananchi wa Kizimkazi, Wilaya ya Kusini na Mkoa mzima wa Kusini.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo akifungua Tamasha la msimu wa nane la Kizimkazi uwanja wa Kashangae Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Tamasha la Kizimkazi miaka michache ijayo litakuwa na mchango muhimu wa kuvutia wageni Zanzibar pia linakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuongeza vivutio vya utalii nchini kupitia matamasha mbalimbali .
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amefurahishwa na ubunifu wa Tamasha hilo kwa kulitumia kuhamasisha maendeleo katika sekta ya afya, huduma kwa makundi maalum, miundombinu, biashara, ujasiriamali na kuimarisha elimu Mkoa wa Kusini.
0 Comments
Karibu!