Na. Kasumal Rashid
Mh. Diwani wa kata ya Kalya, ndg. Jackson Fredrick Thomas amezungumza kuwa, hana mpango wa kugombea nafasi ya ubunge, wa jimbo la Kigoma kusini lililopo wilaya ya Uvinza katika mkoa wa Kigoma. Amesema hayo kwenye grupu la WhatsApp liitwalo UVCCM (W) UVINZA, baada ya kuwa na uvumi mkubwa mtaani na mitandaoni, kuwa ataingia katika kinyang'anyiro cha kugombea ubunge mwaka 2025. Diwani huyo nje na nafasi ya Udiwani, pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza, ni mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Kigoma na mjumbe kamati tendaji ALAT Taifa.
0 Comments
Karibu!