MIAKA 10 BILA ZAHANATI

Zahanati ya kijiji cha LufubuNa: Kasumal Rashid

    Lufubu ni kijiji kinachopatika kata ya Kalya, tarafa ya Buhingu wilaya ya uvinza, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Kijiji cha Lufubu kilipata usajili mwaka 2012, kutoka katika kijiji cha Kashagulu, kijiji hicho kina vitongoji vipatavyo vitatu. 

    Kijiji cha Lufubu kilianzisha ujenzi wa zahanati mnamo miaka ya 2019 kwa nguvu za wananchi, kwa kuamini serikali kuu itaonajuhuhudi zao, na kuweza kuingiza pesa kwa eneo la kukamilisha. Kutokana na juhudi za wananchi walizozionyesha, serikali iliiwekea pesa zahati ya kijiji cha Lufubu kiasi cha milioni hamsini, kilichothibitishwa na Mh. Diwani ndugu, Jackson Fedrick Thomas Mateso katika mkutano wa hadhara ulioganyika katika kijiji hicho.

    Kasumal alipoongea na Mh. Mwenyekiti wa kijiji cha Lufubu, ndugu Maghembe juu ya zahanati hiyo mwenyekiti alizungumza kuwa, nikweli zahati yake ilipewa pesa kiasi  cha shilingi milioni hamsini. Lakini jambo halielewi mpaka sasa tangu pesa hizo zimeingia, hajui ni kitu gani chochote kinachoendelea kwani mambo yote yanaendeshwa, na viongozi na watalaamu kutoka Wilayani. Pia aliendelea kusema kuwa vibarua na fundi mkuu (Foreman), bado wanadai pesa na field wamesha ondoka na amebaki fundi mkuu pekeyake kwani milioni hamsini imekwisha lakini vilevile  zahanati hiyo haina choo.

Post a Comment

0 Comments