WANAFUNZI WAGEUKA KUWA FUNZA

Shule ya msingi KampisaNa: Kasumal Rashid

    Wanafunzi wa darasaawali shule ya msingi Kampisa, wageuka funza baada ya jengo la darasa moja la awali kutokukamilika, kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na kufanya watoto kusoma nje kwa nyakati zote za msimu wa mwaka. 

    Kasumal alipotembelea shule hiyo, alkuta boma moja lililoishia kwenye renta, pia aliongea na baadhi ya walimu wa shule hiyo juu ya hali ile alioikuta. walisema kuwa jengo lile lipo tangu mwaka 2019, na lilijengwa na nguvu ya wananchi na mpaka sasa wanasikia tu litamaliziwa lakini mpaka leo bado halitazamwi. Kasumal pia aliongea na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Kashagulu, walisema kuwa pesa chache za  kukamilisha jengo lile zimeshatengwa, na zipo kwa mtendaji wa kijiji cha Kashagulu.

Post a Comment

0 Comments